HOTUBA YA WAZIRI WA KILIMO NA CHAKULA MHE. CHARLES N. KEENJA (MB.)
WAKATI WA UZINDUZI WA BODI YA WAKURUGENZI WA BODI YA PARETO, KATIKA UKUMBI WA
BODI YA CHAI, TAREHE 24 AGOSTI, 2002,
DAR ES SALAAM
Mwenyekiti
wa Bodi, Mhe. Hassy Kitine,
Ndugu
Wajumbe wa
Bodi,
Awali ya yote napenda
nichukue fursa hii kuwashukuru kwa kunialika
kuja kuzindua Bodi yenu. Napenda kuchukua nafasi hii pia kumpongeza
Mwenyekiti na
Wajumbe wote wa Bodi kwa
kuteuliwa kuunda Bodi ya Pareto.
2. Ndugu Mwenyekiti wa Bodi, napenda nichukue nafasi hii kuongelea masuala
mbalimbali yanayohusiana na maendeleo
ya zao la pareto nchini. Masuala nitakayogusia ni pamoja na; upanuzi
wa kilimo cha pareto nchini, usindikaji wa zao
hilo, usimamizi wa maendeleo ya
zao la pareto na majukumu ya
Wizara katika kuhudumia na maendeleo
ya zao la pareto.
3. Ndugu Mwenyekiti, kabla sijaendelea
na hotuba
yangu naomba kwanza niwakumbushe majukumu ya Bodi ya
Pareto, kulingana na sheria ya pareto
ya mwaka wa 1997. Baadhi ya majukumu
hayo ni;
-
Kumshauri Waziri kuhusu
hatua za kuchukua kukuza, kuendeleza na
kudhibiti zao la pareto (Pyrethrum industry).
-
Kupokea, kuzingatia na kumshauri Waziri kuhusu mapendekezo
yoyote yatakayotolewa na wazalisaji wa
pareto au Umoja wao kwa maslahi
ya zao la pareto.
-
Kupokea na kuzingatia maombi kwa ajaili ya
kuzalisha pareto.
-
Kufanya au kugharamia utafiti
na majaribio
moja kwa moja au kupitia wakala katika jambo
lolote linalohusiana na zao la pareto.
-
Kutoa leseni na
kuamua mazingira ya kutoa leseni
hizo.
-
Kutengeneza kanuni kwa ajili ya kudhibiti visumbufu
na magonjwa.
-
Kutokana na uwezo iliyopewa na sheria, kufanya
yale yote ambayo Bodi inaona
ni lazima kwa kuendeleza zao la pareto.
Nimeanza kwanza kwa kuainisha majukumu ya Bodi
ili tuelewane vizuri katika mambo tunayokusudia kuyafanya.
3. Ndugu Mwenyekiti, kazi ya
kwanza ya Bodi ambayo itabidi muifanye mara moja
ni, kuangalia
upya muundo wa Bodi ya
Pareto katika ngazi zake zote ili
kuona
4. Eneo jingine ambalo
linabidi kutiliwa mkazo ni
kuhakikisha kilimo cha pareto kinapanuka na tija inaongezeka
kuliko ilivyo sasa. Kwa sasa uzalishaji
kwa eneo
ni wastani wa kilo 300 kwa hekta wakati tija
inayowezekana ni wastani wa kilo 600 kwa hekta. Kwa hiyo, kazi iliyo
mbele yenu ni kuhakikisha
watendaji katika ngazi zote wanasimamia
uzalishaji kwa kufuata kanuni za kilimo bora
cha pareto. Mabwana shamba itabidi wapewe mafunzo ya kutosha
kuhakikisha wanakielewa na kukisimamia
ipasavyo kilimo cha pareto.
5. Ndugu Mwenyekiti, changamoto iliyo
mbele yenu ni kuhakikisha
wakulima wanapata pembejeo za kilimo
kwa wakati. Itabidi Bodi ifanye kazi
kwa karibu
6. Eneo jingine muhimu
ni soko
la uhakika la
7. Ndugu Mwenyekiti, kuna taarifa
pia kuwa pareto ya
msimu uliopita bado iko mikononi
mwa wakulima. Ni lazima Bodi ihakikishe pareto yote
ya msimu uliopita inaondoka mikononi mwa wakulima
ili isichanganywe na pareto ya
msimu huu na kusababisha kushuka kwa ubora
wake. Ni matarajio
yangu kuwa katika mkutano wenu wa leo mtaweka mkakati
wa kushughulikia jambo hili na
kuhakikisha tatizo hili halitokei tena.
8. Ndugu Mwenyekiti, kuna tatizo
la uwezo mdogo wa kiwanda
kilichopo cha kuengua pareto. Hili ni eneo linalohitaji kupewa kipaumbele katika mipango yenu ya kuendeleza
zao la pareto. Kuwepo kwa viwanda
vya kuengua na kuchuja pareto
kutasaidia kuimarisha soko la pareto nchini. Aidha, pareto
iliyochunjwa ina soko la uhakika nje ya nchi. Bodi hii itabidi kubuni mbinu mbalimbali
za kuvutia wawekezaji katika viwanda vya aina
hii.
9. Mhe. Mwenyekiti,
10. Ndugu Mwenyekiti, Wizara yangu
mwaka huu imeanza kutekeleza Mkakati wa
Kuendeleza Sekta ya Kilimo. Programu za Kutekeleza Mkakati huu tayari
zimeandaliwa.
Bodi ya Pareto inabidi iwe na mpango wake ambao utakuwa ni
sehemu ya utekelezaji wa Mkakati. Kwa mfano, katika
msimu wa
2002/2003 uzalishaji wa zao la pareto unatakiwa
kuongezeka kwa asilimia 14.
11. Jambo jingine la kupewa uzito wa juu ni
matumizi ya fedha za Bodi. Lazima Bodi ya Wakurugenzi
ihakikishe sehemu kubwa ya Bajeti
inatumika katika shughuli zinazomnufaisha mkulima moja kwa moja. Aidha, fedha inabidi zitumike
kwa kufuata
mpango maalum na kwa shughuli
iliyokusudiwa.
Wizara yangu itasaidia kutafuta ufumbuzi wa
matatizo ya ukosefu wa fedha
pale yanapojitokeza, lakini
kwa Bodi ambazo zinafuata kanuni za matumizi
ya fedha na zile zenye
mipango mizuri ya utekelezaji.
12. Mwisho, napenda kuwahakikishia ushirikiano wa Wizara
yangu katika autekelezaji wa shughuli mbalimbali za kuendeleza zao
la pareto. Nitapenda Bodi hii iwe mfano
mzuri wa
kutafuta ufumbuzi wa matatizo badala
ya kuyaainisha tu. Ni matarajio yetu kuwa Bodi ya
Pareto itatekeleza majukumu
yake kulingana na sheria
na kanuni zilizopo za kuendeleza
zao la pareto nchini. Pale mtakapokwama tafadhali
tuwasiliane mara moja bila kuchelewa.
13. Baada ya kusema
hayo, sasa natangaza kwamba Bodi Mpya ya
Pareto imezinduliwa rasmi. Nawatakia kazi njema ya
kuendeleza zao la pareto.
Asanteni Sana kwa Kunisikiliza