HOTUBA YA WAZIRI WA KILIMO NA CHAKULA, MHESHIMIWA
CHARLES N. KEENJA (MB.) WAKATI WA
KUFUNGUA SEMINA YA KILIMO YA MKOA WA MOROGORO TAREHE 21 NOVEMBA, 2003
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuchukua fursa
hii kukupongeza sana wewe kwa uongozi wako na wa viongozi wengine wa Chama cha
Mapinduzi na Serikali yake kwa juhudi mnazofanya kwa lengo la kuharakisha
maendeleo ya Wananchi wa Mkoa huu. Mkoa wa Morogoro una rasilimali nyingi ambazo zikitumiwa vizuri,
unaweza kuendelea kwa kasi kubwa
2. Mwaka
juzi, mwaka
wa 2001, niliutembelea mkoa wa Morogoro kwa siku
14. Mkuu wa
Mkoa alinitembeza akanionyesha mabonde yenye rutuba na
3. Lengo langu la kutembelea mkoa wa
Morogoro kwa siku 14, ambazo ni nyingi sana, lilikuwa kubaini fursa za
maendeleo katika kilimo na kushirikiana na uongozi wa Mkoa kubuni mikakati ya
kuzitumia kwa maendeleo ya wakazi wa mkoa wa Morogoro na Taifa kwa jumla. Malengo yangu hayakutimia lakini naendelea
kuwa na matumaini kwamba siku itakuja ambapo wakazi wa
mkoa huu watatumia utajiri walionao kwa manufaa
4. Mheshimiwa Mwenyekiti,
suala moja ni la uhakika kabisa. Haitatokea wananchi wa
Mkoa huu wakazinduka ghafla wakainua majembe na kuanza kulilima eneo lote la
mkoa huu. Tukisubiri
5. Mheshimiwa Mwenyekiti,
tunajua kwamba Mkoa wa Morogoro una rasilimali nyingi
za ardhi nzuri, kubwa na inayofaa kwa kilimo.
6. Tukiunda
vikundi vya wananchi katika vijiji na tukavishirikisha
na watumishi waliopo na kuvipa mafunzo, tutaweza kuhakikisha kwamba kila
familia inapimiwa eneo la ardhi la kukidhi mahitaji yake na wala hatutakuwa tukifanya
jambo jipya kwa kuwa limeshafanyika kwa mafanikio katika baadhi ya mikoa humu
nchini.
7. Hatua
ya kuhakikisha kwamba kila mwananchi ana ardhi ya kutosha na
kwamba vijana wana ardhi
8. Baada ya wananchi kupata ardhi ndipo
tunapoanza kazi muhimu ya kutafsiri au kuanisha kilimo cha wananchi wa maeneo mbalimbali ya mkoa wa Morogoro. Vision (taswira) ya mkoa ni nini? Katika
Mkakati wa Kuendeleza Sekta ya Kilimo tunasema kwamba,
“Ifikapo mwaka wa 2025 kilimo chetu kiwe cha kisasa, cha kibiashara,
chenye tija, chenye faida na kinachohakikisha matumizi endelevu ya maliasili
zilizopo na chenye kushirikisha sekta nyingine”. Maana yake ni kwamba
ifikapo mwaka 2025 kilimo chetu kitakuwa cha kisasa, chenye tija na faida. Kwa kuwa Vision hii ni
ya Kitaifa itabidi mkoa wa Morogoro uichukue ilivyo na kuichambua na kuifafanua
ili ioane na matakwa ya wananchi wa mkoa huu na mazingira yake.
9. Kilimo chetu ni sharti kitimize mambo yafuatayo:
Pili:
kilimo chetu ni sharti kitupatie malighafi za viwanda
vyetu vilivyopo na vitakavyojengwa. Kwa
kawaida, nchi inapoanza kuendelea, hujenga viwanda vya kusindika mazao ya
kilimo na baadaye viwanda vya aina nyingine. Uzalishaji wetu wa
mazao ya aina zote bado uko chini
Tatu:
tunalazimika kulima mazao ambayo tutayauza nje ili
tujipatie fedha za kigeni. Kwa wastani, sekta ya kilimo huchangia theluthi mbili za mapato
yetu ya fedha za kigeni.
-
Kilimo kingeweza kutoa mchango mkubwa
zaidi
-
Bei za mazao mengi katika soko la
dunia zimeshuka
Nne: kwa kutekeleza hayo niliyotangulie kueleza,
kilimo kitatoa ajira kwa wananchi na kuchangia kwa kiwango kikubwa katika
kupunguza umaskini.
10. Mkoa wa Morogoro
unaongoza kwa kilimo cha miwa na uzalishaji wa sukari. Hali hii itaendelea, hususan shamba jipya la
Ruipa litakapoanza kuendelezwa na Mtibwa
watakapoendeleza eneo kubwa waliloongezewa na Serikali. Kilimo cha miwa kinawapa wananchi wa Mkoa wa Morogoro fursa ya kuchangia katika uzalishaji wa
miwa
11. Nje
ya kilimo cha miwa na usindikaji wa sukari, Mkoa wa
Morogoro hauna jingine la kujivunia.
Maeneo mengine ya nchi yakilalamika juu ya upungufu wa
chakula, Morogoro nao wamo na mkoa hauna mazao ya biashara ya kujivunia. Hali hii ni lazima
ibadilike na ifanyike hivyo haraka.
12. Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa,
nakusifu
13. Tumekubaliana kwamba mahali pa kuanzia ni kuhakikisha kwamba kila mkulima ana shamba kubwa
linalokidhi mahitaji yake. Ardhi
ndiyo rasilimali kuu katika kilimo na asiyekuwa nayo
hawezi kuwa mkulima. Hatua ya pili ni kuandaa mfumo wa usimamizi na utoaji elimu au ujuzi
unaomshirikisha mkulima na, kwa hiyo unaomfikia. Katika maeneo mengi nchini, wananchi
wamejiunga kwenye vikundi vyao, vinavyoongozwa na
vinavyoshirikisha viongozi na wataalam wa ngazi inayohusika na vikundi hivyo
vimekuwa na mafanikio makubwa
14. Inabidi yawepo mambo yaliyopangwa
kufanywa na yaliyowekewa utaratibu wa
kuyatekeleza. Mambo hayo yaamuliwe na
wananchi wenyewe kupitia kwenye vikundi vyao chini ya ushauri wa uongozi
na wataalam
wao. Inabidi kuwa waangalifu ili uongozi usijichukulie madaraka ya kutoa amri na
vitisho. Lengo la uongozi ni kuelekeza, kushauri, kulea na kuwezesha. Lakini uongozi unapaswa pia kuvisaidia vikundi
kutekeleza maamuzi na maagizo
15. Shughuli
zitakazofanywa na vikundi zitaainishwa kwa ukubwa,
mahitaji na jinsi ya kuyapata na nafasi ya kila mshiriki katika kutekeleza
sehemu yake ya shughuli husika. Kwa
maneno mengine, utaandalaiwa mpango wa kikundi
utakaoonyesha mahitaji ya kuutekeleza lakini utakaoonyesha pia manufaa
yatakayotokana na kutekelezwa kwa mpango huo kwa kikundi na kwa kila
mshiriki. Manufaa yanavyozidi kuwa
makubwa kwa washiriki ndivyo watakavyovutiwa kushiriki
na kuchangia katika kufanikisha shughuli za kikundi.
16. Mipango ya
vikundi vyote katika Kata ikiunganishwa, tutapata mpango wa
kata na mipango ya kata zilizoko katika Wilaya ikiunganishwa, tutapata mpango
wa wilaya au “District Agricultural Development Plan” (DADP). Serikali imekwishaagiza kila wilaya kuandaa
mpango wake wa Maendeleo ya Kilimo na mipango hiyo
ndiyo itakayotengewa fedha kutoka kwenye bajeti ya Serikali na kutoka kwa
Washirika wetu wa maendeleo. Katika
mwezi wa Julai, 2003 utekelezaji wa PADEP ulianza
rasmi na mpango huo utashirikisha Wilaya 28.
Serikali inakusudia kuchukua mkopo wa ADB ambao
utagharimia DADPs katika wilaya nyingine 28 na Benki ya Dunia, IFAD na FAO wako
nchini hivi sasa wakiandaa mpango wa kufikisha utaalam wa kilimo kwa
wakulima. Kwa kifupi, fedha zitapatikana
kwa watakaopanga lakini ni kweli pia kwamba kwa wale
ambao hawatapanga wataachwa nyuma.
17. Suala la nne muhimu linahusu mazao ya
kulimwa, utaalamu wa kuyalima na kuyaandaa kwa matumizi yetu au kwa soko. Kwa upana, tumekubaliana kwamba tutalima
mazao ya chakula na ya biashara kwa sababu ambazo
tumeziainisha. Lakini haitoshi
kuzungumzia mazao kwa upana huo inabidi tuangalie
mazingira yetu na kuamua ni mazao gani yanayostawi katika mazingira hayo na
kuchagua yale yenye manufaa makubwa zaidi ndiyo tukazanie katika
kuyazalisha. Mkoa wa Morogoro uko karibu
na Bandari na Kiwanja cha Ndege cha Dar es Salaam jambo ambalo linatupa fursa
ya kuandaa mipango yetu ya uzalishaji kwa kulenga masoko yaliyoko nje ya mipaka yetu. Mazao kama paprika,
ndizi, pamba n.k. yanatajwa lakini hakuna mipango iliyoandaliwa na kubadilisha
ndoto kuwa ukweli.
18. Uzalishaji ni lazima ulenge mahitaji
ya ndani ya nchi na masoko ya nje na ufanywe kwa makusudi na siyo
19. Yapo mambo ambayo tunayajua lakini hatuandai mipango ya
kuyafanya. Tunajua, kwa
mfano, kwamba tungeweza kuongeza uzalishaji kutoka eneo linalolimwa hivi sasa
kwa hadi mara tano (x5). Tunajua kwamba
asilimia karibu 40 ya mazao tunayozalisha yanapotea kwa
kuharibiwa na wadudu
20. Tunalalamikia mvua zisiponyesha na
zinaponyesha. Tunatumia
sehemu ndogo tu ya mwaka katika uzalishaji. Mkoa wa Morogoro una
21. Mwisho, Mkoa wa Morogoro una mashamba mengi makubwa yaliyotelekezwa. Tumeomba
22. Mheshimiwa
Mwenyekiti, naomba nimalizie kwa
kusisitiza kwamba ili tupate maendeleo katika kilimo tunahitaji:
·
Kuweka mfumo wa usimamizi, na
uhimizaji.
·
Tunahitaji kuandaa mipango ya uzalishaji
itakayoonyesha mahitaji na manufaa yatakayopatikana.
·
Inatubidi kuchagua mazao kwa
kuzingatia mazingira yetu, mahitaji yetu na ya soko la ndani na la nje na
tunapaswa kuzalisha kwa nidhamu na kwa kuzingatia mahitaji ya soko.
23. Uongozi ni muhimu
24. Inabidi tuangalie zana wanazotumia wakulima katika kilimo. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kwamba “
25. Tunatarajia
kwamba tukichukua hatua sahihi, mkulima mdogo atakua kutoka uzalishaji wa kujikimu na kuwa mzalishaji wa kibiashara – anayezalisha
kwa ajili ya soko. Aidha, tunalenga
kuwawezesha watu wenye ujuzi na rasilimali kuwekeza
katika kilimo cha mashamba makubwa ambayo yataingiza teknolojia za kisasa za
uzalishaji na ambayo yatazalisha kwa wingi kwa ajili ya soko.
26. Mheshimiwa
Mkuu wa Mkoa, napenda kuchukua fursa hii kukuhakikishia wewe na
Wananchi wa Mkoa wa Morogoro kwamba Serikali inatambua sana uwezo wa Mkoa wa
Morogoro wa kuwa “grain basket” ya Tanzania na nawaahidi ushirikiano
katika kuwapatia utaalam na rasilimali za kuwekeza. Mkoa una Vyuo Vikuu Viwili, vituo vya Utafiti
na Vyuo vya Kilimo – Mnazo rasilimali nyingi na za
aina zote. Zitumieni! Sharti moja tu ni
kwamba mnapaswa kuamua mnaelekea wapi ili wengine washirikiane nanyi
kuwawezesha kuelekea huko. Miaka iliyopita Mkoa haukuonyesha ari ya kuchukua hatua za
kuharakisha maendeleo ya wananchi wenu.
Naanza kuona mabadiliko na tungependa kuwa
sehemu ya mabadiliko na mafanikio hayo.
Semina hii ni kielelezo cha mabadiliko hayo.
27. Baada ya maneno hayo machache, sasa natamka kwamba semina yenu
imefunguliwa rasmi.