SALAAM ZA WAZIRI WA KILIMO NA CHAKULA
MHESHIMIWA CHARLES N. KEENJA (MB.) WAKATI
WA UFUNGUZI WA MKUTANO WA NNE WA
SEKTA YA PAMBA JIJINI MWANZA
TAREHE 18 – 19 MACHI, 2003
Mheshimiwa George Kahama (Mb.), Waziri wa Ushirika
na Masoko,
Mheshimiwa Daniel Ole Njoolay,
Mkuu wa
Mkoa wa Mwanza,
Mheshimiwa Raphael N. Mlolwa,
Mwenyekiti wa
Bodi ya Pamba,
Mheshimiwa Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza,
Waheshimiwa Mawaziri,
Waheshimiwa Wabunge,
Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa,
Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya,
Waheshimiwa Viongozi wa Serikali,
Waheshimiwa Wageni Waalikwa,
Mabibi na Mabwana.
Mhe. Waziri wa Ushirika na Masoko, napenda kuchukua nafasi hii kukushukuru
kwa kukubali kuwa mgeni rasmi
wa mkutano huu wa nne
wa Sekta ya Pamba. Wewe ni Mdau na Kiongozi muhimu
katika sekta hii na tunaamini
kwamba uongozi wako katika mkutano
huu, utatuwezesha kufanya maamuzi ambayo yataiwezesha sekta hii muhimu
kukua na kuchangia katika kuondoa umaskini miongoni mwa wakulima
wa pamba na kuongeza pato
la Taifa. Tunakushukuru
2. Ndugu Mgeni Rasmi, tulipokutana
mwaka wa
2002 uzalishaji wa pamba ulikuwa marobota
282,000. Katika
mwaka huu, uzalishaji umefikia marobota 354,000 sawa na ongezeko
la asilimia 29.
Ninapenda kuchukua fursa hii kuwashukuru
wakulima, wafanyabiashara na wadau
wengine wa zao la pamba kwa
mafanikio yaliyopatikana. Wizara yangu kupitia Bodi
ya Pamba na kwa kushirikiana na Serikali za Mitaa,
itaendelea kuhimiza kilimo cha pamba ili kifikie lengo
la marobota 750,000 ifikapo
mwaka wa 2006/2007.
3. Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati tukiwapongeza wakulima kwa kuongeza
uzalishaji wa pamba, inatubidi tutambue na kukubali
kwamba uzalishaji wa pamba kwa
eka moja bado ni mdogo
4. Kuongeza tija katika kilimo cha pamba ni
njia sahihi ya kupunguza umaskini
na kuwatajirisha wakulima. Katika msimu wa 2004/2005 Wizara za Kilimo na
Chakula na Ushirika na Masoko
na Bodi ya
Pamba, tutafanya kampeni kubwa ya
kuongeza uzalishaji kwa eneo kwenye
maeneo yote yanayolima pamba. Bodi ya Pamba itaandaa
kampeni hiyo kwa kushirikisha
Halmashauri zote za Wilaya zinazohusika.
5. Bei za Pamba kwenye soko
la dunia ziko chini
6. Bei ndogo ya pamba inatokana
pia na
kuuzwa kwa pamba bila ya
kuongezewa thamani kwa kusindikwa. Baadhi ya viwanda vyetu vya nguo
vimekwisha binafsishwa. Tunawaomba wale waliovinunua wavikarabati haraka ili
vianze uzalishaji wa nyuzi na
nguo. Kiwanda cha MWATEX kiliwahi kuwa na sifa ya kuzalisha
nguo zilizopendwa
7. Kilimo chetu cha
pamba kinakabiliwa na tatizo
la matumizi ya jembe la mkono kulimia. Tunawaomba Serikali za Mitaa na Vyama vya Ushirika kuhimiza
8. Kuanzia msimu wa 2004/2005 ukanda
wote wa Magharibi
utatumia aina moja ya mbegu
inayojulikana
9. Kwa kifupi, mipango ya uzalishaji
wa pamba
katika miaka ijayo inapaswa kulenga:
(a)
Kuongeza uzalisha
kwa eneo
kwa kufuata masharti ya kilimo
bora.
(b)
Kushirikiana na Serikali za Mitaa Vyama
vya Ushirika, Vikundi vya Wananchi
na wananchi wenye uwezo, kuongeza
matumizi ya wanyamakazi na matrekta kupunguza uzito wa kazi
za kilimo na usafirishaji wa pembejeo na
mazao.
(c)
Kuhakikisha kwamba
pamba yetu inarudia ubora wa hali ya juu,
(d)
Kuhimiza usindikaji
wa pamba
ili kuiongezea thamani na kuongeza
ajira.
(e)
Kuweka utaratibu wa kupata
mbegu bora na ya aina
inayopendekezwa na kuifikisha kwa wakulima.
10.
11. Mheshimiwa Waziri, baada ya maelezo haya mafupi,
sasa nakuomba utufungulie mkutano huu wa wadau wa pamba
na kisha uuongoze kwa kuwa
Mwenyekiti wetu.
Asanteni kwa kunisikiliza.