HOTUBA
YA MHE. CHARLES N. KEENJA (MB.) YA KUMKARIBISHA MGENI RASMI
KUHITIMISHA MAADHIMISHO YA NANENANE, 2002 MOROGORO, 08 AGOSTI, 2002
Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kuchukua muda huu
kukushukuru
2. Mheshimiwa
Mgeni Rasmi,
maadhimisho ya Nane Nane yanafanyika kwenye viwanja hivi kwa
mara ya tatu mfululizo kutokana na uamuzi uliofanywa na TASO wa kujenga eneo
hili, ili liwe kituo cha Kanda ya Mashariki cha Maadhimisho ya Nane Nane.
3. Pamoja na
mafanikio mazuri yaliyopatikana, bado iko kazi kubwa ya kuendelea kujenga
majengo ya kudumu na kuweka utaratibu wa kuyatumia mwaka mzima. Baadhi ya washiriki wanasita kuwekeza kiasi
kikubwa cha fedha kwa hofu kwamba mwakani watatakiwa
kuhamia kwenye kituo kingine.
4. Namshukuru
5. Mheshimiwa
Mgeni Rasmi,
Maonyesho ya kilimo yanaonyesha dhahiri kwamba tunao ujuzi unaotakiwa wa kumwezesha mkulima kupata tija kubwa zaidi katika
kilimo. Vituo vyetu vya Utafiti na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, vimezalisha mbegu
nyingi zenye sifa bora za kutoa mazao mengi kwa eneo, ukinzani wa magonjwa,
uvumilivu wa ukame na viini vya lishe bora.
Kazi iliyo mbele yetu ni kuzalisha mbegu hizo
kwa wingi na kuzifikisha kwa mkulima mapema iwezekanavyo. Nachukua nafasi hii kuyashauri makampuni
ambayo yamekuwa yakiagiza mbegu kutoka nje kuchukua hatua za haraka za kuzalisha
mbegu hizo humu nchini
6. Kazi nyingine ambayo itafanyika
katika mwaka ujao ni kusambaza mbinu za ugani na
utafiti shirikishi na mbinu nyingine zilizojaribiwa kwa mafanikio za kufundisha
kilimo bora, kwa mfano, shamba darasa.
Mfumo wa kuoanisha utafiti na huduma za ugani
utaangaliwa upya na kuimarishwa.
7. Kazi ya tatu itakuwa ni kuhakikisha upatikanaji wa pembejeo na zana za kilimo za
kutosha na kwa wakati. Tunatambua kwamba
tatizo kubwa ni uwezo mdogo wa mkulima wa kununua
pembejeo na zana hizo bila mkopo. Katika
hotuba yako ya kuahirisha Mkutano wa Bunge la Bajeti
tarehe 31 Julai, 2002, uligusia suala la vyombo vya fedha kutenga sehemu ya
fedha zao kukopesha kilimo.
Tunakushukuru kwa maelekezo hayo na
tutashirikiana na Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya
8. Kazi ya nne
ni kuhakikisha kwamba mazao yanayozalishwa yatakuwa ya ubora wa kimataifa ili
yaweze kupata bei nzuri katika masoko ya ndani na nje ya nchi.
9. Kazi ya tano ni
kuendeleza juhudi za kufufua na kuongeza
10. Mheshimiwa
Mgeni Rasmi, Watanzania
wengi hawana imani kwamba kilimo chetu kinaweza kukua kwa
viwango vya kuridhisha. Sisi katika
Sekta ya Kilimo tumeandaa mipango na utaratibu ambao
unatupa matumaini kwamba kasi ya kukua kwa uzalishaji katika kilimo itaendelea
kuongezeka kutoka asilimia 5.5 ya mwaka jana kuelekea kwenye asilimia zaidi ya
10 katika miaka michache ijayo.
11. Napenda kuchukua nafasi hii
kuwashukuru na kuwapongeza wakulima kwa mchango wao
mkubwa katika maisha na uchumi wa Taifa hili.
12. Baada ya maneno hayo machache, sasa nina heshima kukukaribisha kuzungumza na wakulima,
wafanyabiashara, walaji n.k. na kuhitimisha maadhimisho ya Nane Nane 2002.
Karibu Sana!