Press Release
The Web Kilimo web
Home| Budget Speeches | Publications | Agricultural Statistics | Legislations and Regulations | Web Links
 

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

MINISTRY OF AGRICULTURE AND FOOD SECURITY

Telegrams: KILIMO Dar es Salaam Administration

Telephone: ( 022) 2860326 P.O. Box 9192

Fax: 255(022) 2865312 DAR ES SALAAM

Telex: 41246 KILIMO TZ Tanzania

E-mail: psK@kilimo.go.tz

Kumb. No. EA 19/127/01 April 17, 2008

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Stakabadhi ya Mazao ghalani

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Stephen Wasira ametembelea wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani wiki hii April 16, 2009 kwa lengo la kuona hali ya ununuzi wa zao la korosho.

Akiongea na wakulima wa kijiji cha Magawa wilaya Mkuranga juu ya hali ya soko ya zao la korosho zilizoghani kijijini hapo Waziri Stephen Wasira amewahakikishia wakulima kuwa serikali itahakikisha kuwa korosho za wakulima zinanunuliwa zikiwemo zile zilizoko ghalani na majumbani.

Serikali imekusudia kuanzisha mfumo wa stakabadhi ya mazao ghalani katika mkoa wa pwani ili kuondoa tatizo la ukosefu wa soko la zao la Korosho katika mkoa wa Pwani ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu 2009

Mfumo wa stakabadhi ya mazao ghalani huko Mtwara imefanikiwa kwa kiwango kikubwa ambapo wakulima wa korosho wa Tanzania kwa mara ya kwanza wameweza kulipwa hadi mara tatu kwa kilo moja.

Hatua nyingine zinazochukuliwa katika kuimarisha soko ni pamoja na kuboresha mfumo wa pembejeo ambao utawawezesha wakulima kupata pembejeo kwa wakati, zitakazotumiwa na wakulima ili kuongeza uzalishaji wa korosho zenye sifa ya daraja la kwanza.

Serikali kupitia Bodi ya Korosho Tanzania inatoa ruzuku ya madawa aina ya sulphur kwa kiwango cha asilimia 50 kwa madawa ya maji na asilimia 30 kwa sulphur ya unga ambapo mfuko wa pembejeo wa wilaya utakuwa unachangia asilimia 50 ya gharama za madawa ya kupulizi kwenye mikorosho.

Waziri amewashauri wakulima kutumia sulphur ya maji kuliko ya unga kwa sababu ni nafuu

Kuhusu upangaji wa madaraja waziri wa kilimo ameigiza Bodi ya Korosho Tanzania kuwafundisha Maafisa ugani wa Mkuranga namna ya kupanga madaraja ili wataalamu nao waweze kuwafundisha wakulima kwa lengo la kuhakikisha kuwa korosho zinapenya kwenye soko la ushindani.

Aidha wakulima wa mkuranga nao wameombwa kuweka jitihada ya kulima na kusafisha mashamba yao yaliyo porini katika kuunga mkono juhudi za serikali zinazofanywa za kuwawezesha kupata fedha kupitia zao la korosho.

Katika ziara hiyo waziri ametumia muda mwingi katika kuwahamasisha vijana waingie kwenye shughuli za kilimo kwa sababu soko la mazao hususani embe na mazao mengine kama vile mboga na matunda lipo Dar es salaam.

Serikali inaangaliwa uwezekano wa kuwasaidia vijana waliojiunga kwenye vikundi vya uzalishaji mali katika kilimo kwa kuwapatia matrekta madogo ya mkono ili waweze kuzalisha mazao ya chakula na biashara.

Rainard Kayombo

Afisa Mawasilinano-Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika

Wasiliana nasi Simu: 2861319 au 0772557

 

 
 
Speeches| Publications | Agricultural Statistics | Legislation and Regulations | About us|Contact us
Copyright 2008, Ministry of Agriculture Food Security and Cooperatives All rights reserved.