Walengwa wa mikopo ya
pembejeo za kilimo na mifugo ni wakulima au wafugaji kupitia kwenye vikundi,
wakulima au wafugaji binafsi, Vyama vya Msingi, Mifuko ya Pembejeo ya Wilaya,
Vyama vya Kuweka na Kukopa (SACCOS) na mawakala wa kusambaza pembejeo wenye
uzoefu usiopungua miaka miwili.
Pembejeo zinazoweza kuombewa mikopo ni mbolea za aina
mbalimbali za viwandani, mbegu bora, dawa za tiba na chanjo za mifugo,
vyakula vya mifugo, dawa za kuhifadhi mazao ya kilimo na mifugo, sumu za
magugu, vifungashi vya mazao ya kilimo na mifugo na zana ndogondogo za
kilimo na mifugo za mikono au zinazokokotwa na wanyamakazi, kununua matrekta
mapya na kukarabati matrekta mabovu.