|
| |
|
Mikopo ya Pembejeo za Kilimo na
Mifugo
|
|
|
|
|
Mfuko wa Pembejeo unatoa mikopo ifuatayo,
mikopo ya pembejeo za kilimo na mifugo ambazo ni mbolea za aina mbalimbali
za viwandani, mbegu bora, dawa za tiba na chanjo za mifugo, vyakula vya
mifugo, dawa za kuhifadhi mazao ya kilimo na mifugo, vifungashi vya mazao
ya kilimo na mifugo na sumu za magugu, mikopo ya kununua matrekta mapya,
mikopo ya kuanzisha vituo vya kukodisha matrekta, mikopo ya kukarabati
matrekta, mikopo ya kununua matrekta madogo ya mkono (Power tillers), mikopo
ya zana ndogondogo za umwagiliaji,na zana ndogo ndogo za kilimo kama vile
majembe ya kukokotwa na wanyama kazi (Plau).
1) WALENGWA WA MIKOPO YA KUTOKA MFUKO
WA PEMBEJEO
Walengwa wa mikopo ya pembejeo za kilimo na
mifugo ni wakulima au wafugaji kupitia kwenye vikundi, wakulima au wafugaji
binafsi, Vyama vya Msingi, Mifuko ya Pembejeo ya Wilaya, Vyama vya Kuweka na
Kukopa (SACCOS) na mawakala wa kusambaza pembejeo wenye uzoefu usiopungua
miaka miwili.
2) UTEUZI
WA WAOMBAJI WA MIKOPO
 |
Halmashauri za Wilaya
hutoa tangazo la kuwapo mikopo kutoka Mfuko wa Pembejeo kama
zilivyoainishwa hapo juu.
|
 |
Waombaji watatakiwa
kujaza fomu maalum za maombi na kutoa maelezo binafsi, namba ya simu,
anuani ya makazi na biashara/shamba ikiambatanishwa na mchanganuo wa
matumizi ya mkopo anaoomba (Business plan), kivuli cha leseni hai ya
biashara ya pembejeo kwa wafanya biashara na kivuli cha hati miliki ya
dhamana ambacho mmiliki wake ndiye anayeomba mkopo.
|
 |
Maafisa Kilimo/Mifugo
wa Wilaya huthibitisha shughuli zinazoombewa mikopo katika wilaya husika
kabla ya kuziptisha
|
 |
Fomu za maombi
zilizohakikiwa pamoja na vielelzo vinavyohitajika hupitishwa na
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya/Miji/Manispaa/jiji.
|
 |
Fomu za maombi na
vielelezo vinavyohitajika pamoja na mahitaji ya pembejeo ya Wilaya
husika hutumwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Pembejeo katika muda
maalum kama ifuatavyo;
|
-
Machi
hadi Mei,
mikoa ya Ruvuma, Rukwa, Mbeya, Iringa, Dodoma, Singida, Tabora,
Shinyanga, Kigoma, Kagera, Mara na Mwanza.
- Agosti
hadi Septemba,
mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Pwani,
Mtwara, Lindi na Dar es salaam.
 |
Maombi haya huchambuliwa na
kuwasilishwa kwenye kikao cha kamati ya mikopo na baadaye kwenye Bodi ya
Wadhamini wa Mfuko ili yaidhinishwe. |
 |
Maamuzi ya Bodi hutumwa
kwa waombaji na kwenye Halmashauri za Wilaya husika. |
3)
MASHARTI YA MIKOPO
-
Wakulima
na wafugaji binafsi, kampuni na mawakala wa kuuza pembejeo, sharti wawe
na dhamana isiyohamishika yenye hati miliki (Title deed) na
inayokubalika kisheria. Mwombaji sharti awe ndiye mmiliki wa hati
itakayodhamni mkopo. Mmiliki wa dhamana ya mkopo atatakiwa kupata
uthibitisho kutoka ofisi ya ardhi iliko dhamana yake kuhusu uhalali wa
umiliki wake na kwamba haina matatizo yoyote kwa kujaza consent letter.
-
Kwa mikopo ya pembejeo mwombaji awe amefanya biashara ya pembejeo kwa
muda usiopungua miaka miwili.
-
Mifuko ya Pembejeo ya
Wilaya isiyo na dhamana zenye hati miliki itadhaminiwa na Halmashauri za
Wilaya husika.
-
Vyama vya kuweka na
kukopa (SACCOS), vikundi vya wakulima na wafugaji visivyo na dhamana za
hati miliki sharti viwe viwe na akiba ambayo ni sawa na theluthi moja ya
mkopo wanaoomba. Waombaji wa kundi hili watatakiwa kuwa wanachama wa
asasi ya kifedha itakayotoa mkopo kwa niaba ya Mfuko wa Pembejeo.
-
Mwombaji atatakiwa
kulipia gharama za kutathmini dhamana ya mkopo wake pamoja na asilimia
moja (1%) ya mkopo utakaokuwa umeidhinishwa.
-
Kwa mikopo ya matrekta
mapya, mwombaji sharti awe na shamba binafsi lenye ukubwa usiopungua
ekari 50 na awe tayari kutoa huduma ya kukodisha trekta hilo kwa
wakulima wenzake.
-
Mkopaji wa trekta atatakiwa
kulifanyia matengenezo madogo na makubwa trekta litakalonunuliwa kwa
mkopo mara kwa mara kama atakavyoelekezwa na mtengenezaji au muuzaji wa
trekta hilo. Aidha, trekta hilo litakuwa sehemu ya dhamana ya mikopo na
kadi ya uandikishaji (Registration card) itakuwa chini ya umiliki wa
Mfuko mpaka mkopo utakaporejeshwa.
-
Muda wa kurejesha mikopo
ya Mfuko wa Pembejeo ni mwaka mmoja na nusu kwa mikopo ya pembejeo za
kilimo na mifugo, miaka miwili kwa mikopo ya kukarabati trekta, miaka
mitatu kwa matrekta madogo ya mkono (power tiller) na miaka mitano kwa
mikopo ya matrekta mapya.
|
|
| |
|