Mfuko wa Pembejeo ulianzishwa kwa sheria ya Bunge Namba 9 ya
mwaka 1994. Madhumuni ya Mfuko ni kugharimia uagizaji na usambazaji wa
pembejeo za kilimo na mifugo ili kuhakikisha kuwa zinawafikia wakulima
na wafugaji kwa wakati mwafaka.
Ili kutimiza lengo hilo, Mfuko wa Pembejeo unatoa mikopo
inayotozwa riba nafuu kwa ajili kununua na kusambaza pembejeo za kilimo na
mifugo. Aidha, kuanzia msimu wa 2003/2004 Mfuko ulianza kutoa mikopo ya
kukarabati matrekta na kununua matrekta mapya na zana
zake.