1.
Mwombaji atajaza fomu maalum ya maombi inayopatikana katika Ofisi za kilimo
za
Halmashauri za Wilaya na Makao makuu y Mfuko wa Pembejeo, jijini Dar-es-salaam.
2. Fomu za maombi
zilizojazwa na kuambatanishwa na vielelezo vinavyohitajika zitapitishwa na
kuidhinishwa na Afisa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo wa Wilaya na Mkurugenzi
Mtendaji wa Wilaya husika na baadaye kutumwa mapema kwa Mkurugenzi Mtendaji
wa Mfuko wa Pembejeo.
3. Mikopo ya kununua
matrekta inapitia benki, mwombaji sharti atimize yafuatayo:-
·
Awe na dhamana binafsi kwa
jina lake isiyohamishika yenye hati miliki (title deed) na inayokubalika
kisheria.
·
Awe
tayari kutekeleza masharti ya mikopo ya benki itakayotoa mikopo kwa
niaba ya Mfuko wa Pembejeo ikiwa ni pamoja na kufungua akaunti na benki
husika, kulipa asilimia moja (1%) ya mkopo kabla ya mkopo haujaidhinishwa na
kutolewa, na kusajili trekta kwa jina lake na benki au taasisi ya fedha
itakayotoa mkopo.
·
Awe tayari kulifanyia matengenezo madogo na makubwa
trekta litakalonunuliwa kwa mkopo mara kwa mara kama
atakavyoelekezwa na mtengenezaji au muuzaji wa trekta hilo.
4. Muda wa mkopo ni miaka mitatu kwa riba ya asilimia kumi
(10%)