1. Mwombaji atajaza fomu maalum ya maombi inayopatiakana kwenye ofisi
za Halmashauri ya Wilaya/Mji/Manispaa na kweye tovuti ya mfuko. Fomu hii
itapitishwa na Afisa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo wa Wilaya na Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya husika
2.
Afisa Zana katika Halmashauri watashirikiana na mmiliki pamoja na
fundi wake kufanya tathmini ya kiwango cha ubovu wa matrekta hayo katika
maeneo yaliyoanishwa katika
taarifa ya tafiti za awali ya ukarabati. Mapendekezo yazingatie kiwango
cha matengenezo ili gharama za vipuri na fundi zisizidi kiwango cha juu
kinachoweza kutolewa.
3. Mwombaji atachagua Mtengenezaji/Fundi kutoka
kwenye orodha ya kampuni
zitakazoingia mkataba na Mfuko wa Pembejeo. Mtengenezaji/Fundi atafanya
ukarabati chini ya usimamizi na ukaguzi wa Afisa Zana. Mtengenezaji/Fundi
atawajibika kutoa hati ya kuthibitisha ubora wa kazi/matengenezo na
gerentii ya miezi
sita kwa
vipuri vilivyokarabatiwa.
4.
Fomu za maombi pamoja na vielelezo vinavyohitajika zitatumwa kwa
Mkurugenzi Mtendaji, Mfuko wa pembejeo.
5.
Dhamana ya mkopo huu ni kadi halisi ya trekta na mali nyingine
isiyohamishika.
6.
Muda wa mkopo ni mwaka mmoja na nusu kwa riba ya asilimia nane
(8%).
7. Mwombaji sharti awe tayari kutoa huduma
ye kukodisha trekta hilo kwa wakulima
wenzake